Thursday, February 8, 2024

MAFUNDISHO YA MCHUNGAJI S. KUZENZA

 Ilikuwa jumapili ya Tarehe: 2 Feb 2020, Ndani ya FPCT Shalom

MNENAJI: MCH. S KUZENZA
Ujumbe: Namna Mungu anavyozungumza nasi
#MASIKIO YA NDANI
@ Amani ya Kristo huamua ndani yetu
Rumi 8:14
Yer 31:31-33
2 Kor 3:3
=>Dhamiri ndani yetu ndio mahakama inayotoa hukumu ndani yetu
NB: Sheria ya Roho wa Uzima inaandikwa ndani ya roho (dhamira) zetu
Rumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
=>Roho Mtakatifu anatumia Amani ya Mungu ndani yetu kuzungumza nasi, na Amani ya Kristo ndio kiongozi wa akili zetu
Filipi 4:7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Mithali 3:5 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,Wala usizitegemee akili zako mwenyewe
Kolosai 3:15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
#AMANI YA KRISTO -
1. Ndio tuliyoitiwa
2. Inaamua ndani
Efeso 4:1-3
1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu
2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;
3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
#Ili Mungu aendelee kusema nawe hakikisha uwe mtiifu kwake!