Punda kuvalishwa nepi Wajir, Kenya
Kaunti moja ya
Kaskazini mashariki mwa Kenya imechukua hatua zisizo za kawaida kulinda
barabara moja iliotiwa lami, kwa kuwavalisha nepi punda wanaotumia
barabara hiyo.
Mikokoteni yote inayofanya kazi Wajir sasa
italazimika kuweka begi nyuma ya wanyama hao ili kuokota kinyesi chao
kwa lengo la kuhakikisha barabara iko safi.Ni barabara kuu ya kwanza katika historia ya eneo hilo.Wakenya wameenda katika mitandao ya kijamii ili kusambaza uvumi vile punda wa Wajir wanapaswa kufuata sheria hiyo mpya mara moja.
Hii hapa taarifa iliotolewa na serikali ya eneo hilo:
''Tunashukuru mchango unaoletwa na waendesha mikokoteni ya punda kwa uchumi wa Wajir,hatahivyo,mji huo ni sharti usafishwe kila mara.Kutokana na hilo,mumeagizwa kusimamia kinyesi cha punda wenu ili kutochafua barabara.Hakuna Punda atakayeruhusiwa mjini bila mfuko wa kubebea kinyesi kufikia tarehe 29 mwezi Mei''.
Picha mpya za mabaki ya EgyptAir zatolewa
Jeshi la misri limetoa picha za
vifaa vilivyopatatikana wakati wa shughuli ya kutafuta ndege iliyopotea
ya EgyptAir katika bahari ya Mediterranean.
Kati ya picha zilizowekwa ni pamoja na jaketi za kuokoa maisha, sehemu za viti, na vifaa vingine vyenye nembo ya EgyptAir.Ndege hiyo ilikuwa ikitokea mjini Paris nchini Ufaransa ikiwa na watu 66, wakati ilitoweka kutoka kwa mitambo ya radar siku ya Alhamisi.
Wachunguzi nchini Ufaransa wamethibitisha ripoti kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe kuwa moshi ulikuwa kwenye ndege muda mfupi kabla itoweke.
Lakini hata hivyo wanasema kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege bado hakijulikani.
Shughuli hiyo ya kutafuta pia imepata sememu za wanadamu na mizigo.
Sehemu kubwa ya ndege hiyo na visanduku viwili vya kunasa mawasiliano ya ndege havijapatikana.
Serikali ya Ujerumani imeidhinisha mswada unaowaruhusu wagonjwa walio katika hali mahututi kutumia bangi kama dawa kuanzia mwaka ujao.
Mataifa kadhaa ya Ulaya tayari yanatumia bangi kutibu magonjwa kupitia uidhinishaji maalum,huku majimbo kadhaa ya Marekani yakipiga marufuku utumizi wake .