MZEE HEZRON ZACHARIA AKIFUNDISHA VIJANA
Mnakaribishwa katika uzinduzi huo tunatarajia kuuna MKONO wa MUNGU. Waimbaji wengi watakuwepo.
Ninawezaje kushinda dhambi katika maisha yangu ya kikristo?
Jibu: Biblia inazungumzia juu ya vitu hivi tulivyonavyo ili tushinde maisha yetu ya dhambi:
(1) Roho Mtakatifu – kipawa kimojachapo ambacho Mungu ametupa (kanisa lake) kwa ajili ya kuwa na ushindi katika maisha ya kikristo ndani ya Roho Mtakatifu. Mungu anatofautisha mtendo ya mwili na matunda ya Roho Mtakatifu katika wagalatia 5:16-25. katika andiko hilo tunashauriwa kutembea katika uwepo wa Roho Mtakatifu. “waumini wote tayari wamejazwa na Roho Mtakatifu”,lakini hapa tunasisitizwa kupatia nafasi Roho Mtakatifu atutawale na kutuongoza. Hii ina maana ya kuwa tusikilize sauti yake tusije tukatenda mapenzi yetu wenyewe.
Tofauti ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuifanya maishani mwa mtu ni kama ile ya Petro, kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mara tatu, na alikuwa mbeleni ameahidi kumfuata Yesu mpaka kwenye hatari ya kifo angekufa naye. Baada ya kujazwa na Roho alizungumza waziwazi na kwa ujasiri mbele ya wayahudi juu ya mwokozi katika siku ya pentekote.
Unatembea ndani ya Roho ukiwa humzuii anapotaka kujidhihirisha (“kumzima Roho” wathesalonike wa kwanza 5:19) na una kiu ya kujazwa naye kila wakati (Waefeso 5:18-21). Je mtu hujazwaje na Roho Mtakatifu? Kwanza ni kwa mapenzi ya Mungu kama vile ilivyo katika agano la kale. Alikuwa akichagua watu Fulani, kuwajaza kwa ajili ya kutekeleza kazi ama wadhifa Fulani (Mwanzo 41: 38; Kutoka 31:3; Hesabu 24:2; Samueli wa kwanza 10:10; na kadhalika.) Ninaamini kuwa kuna ushahidi katika Waefeso 5:18-21 na Wakolosai 3:16 yakuwa Mungu huchagua kujaza wale wanaojijaza Neno la Mungu kwa kuwa kote kote ni kujazwa uwezo wa Mungu.
(2) Neno la Mungu, Biblia – Timotheo wa pili 3:16-17 inasema ya kwamba Mungu ametupa neno lake ili lituandae katika kufanya kazi njema. Linatufundisha jinsi ya kuishi na cha kuamini, linatufunulia kama tumetenda makosa na kuturudisha katika njia ya sawa. Kama waebrania 4:12 inavyosema Neno la Mungu liko hai na lina nguvu ya kupenya ndani ya nafsi zetu kung’oa lile tatizo ambalo mwanadamu hangeweza kulitatua. Mwandishi wa zaburi azungumzia uwezo wa Neno la Mungu juu ya kubadilisha maisha ya watu katika zaburi 119:9,11,105 na aya nyengine. Joshua aliambiwa siri ya kushinda adui zake (inayoashiria pia vita vyetu vya kiroho) ni kwamba asilisahau Neno la Mungu bali alitafakari usiku na mchana ili akalitimize. Haya aliyatenda, ijapokuwa maagizo yenyewe hayakuwa na uhusiano na mambo ya kivita lakini yakampa ushindi katika vita vya kuimiliki nchi ya ahadi.
Hii ni sehemu ambayo mara nyingi tunaipuuza. Tunapenda kubeba biblia tukienda kanisani ama kusoma aya za kukariri lakini hatuyatilii maanani yale tuyasomayo. Hatuyatafutii nafasi maishani mwetu kiasi cha kutubu dhambi zetu na kumtukuza Mungu kwa kipawa hiki. Tunasoma tu kiasi cha kupata mtazamo Fulani juu ya wokovu lakini hatuongezi juhudi zozote katika kutafakari kwetu mara kwa mara kiasi cha kutufanya tuwe na afya nzuri kiroho.
Ni muhimu sana kwako ufanye tabia ya kusoma neno la Mungu. Kama bado hujazoea basi Roho anakusisitiza uwe na tabia ya kulisoma Neno la Mungu. Nina kushauri uwe na kumbukumbu ya yale uliyoyasoma kwa kuyanakili kwenye daftari lako au kwenye kompyuta. Biblia ndicho kifaa Roho hutumia katika maisha yetu na maisha yaw engine (Waefeso 6:17), ikiwa ni sehemu kubwa ya silaha mojawapo ambayo Mungu hutupa ili tupigane vita vya kiroho (Waefeso 6:12-18)!
(3) Maombi – Hii pia ni njia nyengine ambayo Mungu ametupatia. Njia hii wakristo wengi huitaja tu kwa maneno lakini hawaitumii. Tuna ibada za maombi na nyakati za maombi na kadhalika lakini hatuoni manufaa ya jambo hilo sawa na kanisa la kwanza (Matendo 3:1; 4:31; 6:4; 13:1-3, na kadhalika). Paulo mara kwa mara arudia kueleza vile alikuwa akiwaombea wale aliokuwa akiwahudumia. Lakini tunapokuwa peke yetu hatuitumii njiaa hii. Mungu ametuahidi mambo mazuri ya ajabu kuhusiana na maombi (Mathayo 7:7-11; Luka 18:1-8; Yohana 6:23-27; Yohana wa kwanza 5:14-15, na kadhalika.) Paulo analiongezea mkazo tena katika mafundisho yake juu ya kujiandaa kwa ajili ya vita vya kiroho (Waefeso 6:18)!
Je, ni muhimu kiasi gani njia hii? Tunapomtazama tena Petro, tunaona maneno ya kristo aliyomwambia kabla hajamkana kule Gethsemane. Yesu alipokuwa akiomba Petro alilala. Yesu akamwambia, “Kesheni mkiomba ili msiingie majaribuni: Roho inataka lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41). Wewe pia kama Petro unataka kufanya mema lakini huna nguvu yakutosha kufanyia hayo. Lazima tufuate mausia ya Mungu, tuendelee kumtafuta, tukibisha na kumuuliza… na atatupatia nguvu ile tuitafutayo (Mathayo 7:7 na kuendelea). Lakini lazima tuitilie mkazo njia hii maishani mwetu ndiyo tufaulu. Sisemi ya kwamba maombi ndiyo njia maalum zaidi. La sivyo. Mungu ni wakutisha. Maombi ni kukubali hali zetu za udhaifu, ukuu wa Mungu mwenye nguvu na asiyeshindwa ili tupate uwezo huo huo tuweze kuyafanya yaliyo mapenzi yake (wala si yetu) (Yohana wa kwanza 5:14-15).
(4) Kanisa – Hii ni mojawapo ya njia tunazozifumbia jicho. Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili (Mathayo 10:1). Tunaposoma juu ya habari za safari za wale wamishenari katika kitabu cha matendo ya mitume, hawakuenda mmoja mmoja bali katika makundi, wawili wawili au zaidi.Yesu alisema mahali wawili au watatu wamekusanyika kwa ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao (Mathayo 18:20). Anatuamuru tusiache kukusanyana pamoja kama kawaida za watu wengine zilivyo bali tuutumie wakati wa kuwa pamoja kwetu kwa kutiana moyo katika upendo na matendo mema (Waebrania 110:24-25). Anatuagiza kutubu dhambi zetu mmoja kwa mwingine (Yakobo 5:16). Katika habari za hekima katika agano la kale tunaambiwa ya kwamba chuma hunoa chuma mwenziwe, vivyo hivyo mtu huchangamsha sura ya rafiki yake (Methali 27:17) “kamba ya nyuzi tatu haikatiki rahisi.” “kuna nguvu katika umoja wa wengi (Mhubiri 4:11-12).
MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA NA Msama Promotion. Alex Msama akitoa taarifa za tamasha la pasaka mwaka 2016.
Tamasha hilo limefanyika sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzani, ikiwamo Geita (26/03/2016), Mwanza (27/3/2015) na wilayani Kahama (28/3/2016).
Sehemu hizi zote tamasha imefanyika kama ilivyo pagwa, na waimbaji kama Rozy Mhando, Faustine Mnishi, n.k wa konga nyoyo za watu wengi.
Mashabeki wa nyimbo za injili wakifurahi katika tamasha (CCM Kirumba -Mwanza)
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wa nne kutoka kulia akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipokuwa akimkaribisha rasmi ili kutoa salam zake kutoka kwa serikali.
SEMINA YA PASAKA MARCH 2016
SOMO: MAMLAKA NA NGUVU YA DAMU YA YESU KUSHUGHULIKIA VIFUNGO VYA KIROHO NA VIBALI VYA UTUMISHI
MNANAJI: MWAL. EMANUEL PAUL
Isaya 61:1
Damu ya Yesu inamamlaka na nguvu zote juu ya ukombozi wa mwanadamu kutoka mateka na vifungo Efeso 1:7
VIFUNGO VYA KIROHO
=>Vifungo vya kiroho husababishwa na ulimwengu wa shetani, ulimwengu wa Mungu na mtu binafsi