Saturday, June 25, 2016

Rais Magufuli azindua Mpango mkakati wa kupunguza uhalifu

Rais DK. John Pombe Magufuli leo amezindua mpango mkakati wa kupunguza uharifu nchini huku akilitaka jeshi la polisi kuwasaka kwa udi na uvumba majambazi nchini kote na kisha kuwachukulia hatua stahiki.
Akizindua mpango huo Rais Dk, Magufuli amesema mpango huo wa miaka mitatu ambao utaanza kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Julai Mosi, utafanikiwa tu endapo wananchi watashirikiana kikamilifu na jeshi la polisi , huku akimtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini Ernest Mangu kuhakikisha analisafisha jeshi lake kwa kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafukuza askari wote watakaobainika wanakwenda kinyume na maadili ya kazi zao.
Wakizungumza katika uzinduzi wa mpango huo ambao lengo lake kuu ni kukomesha uhalifu nchini ,wafadhili wakuu wa mpango huo wakiwemo benki ya CRDB ambao wametoa zaidi ya shilingi milioni 320 kujenga kituo cha kisasa cha mawasiliano pamoja na benki ya NMB ambao nao pia wamejenga vituo vya polisi viwili vinavyohama , wamesema ulinzi na usalama ni jukumu la kila mwananchi na kwamba bila usalama na amani hakuna shughuli yoyote ya kijamii na kiuchumi inayoweza kuendelea.
Awali Rais Magufuli alizindua kituo cha kisasa cha mawasiliano kilichopo kituo kikuu cha polisi kanda maalum ya Dar es salaam ambapo akiwa katika viwanja vya biafra alitembelea mabanda mbalimbali ya polisi ili kujifunza zaidi juu ya mpango huo wa kuboresha usalama wa raia.

Friday, June 24, 2016

Waziri mkuu wa Uingereza ajiuzulu

 

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.
Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.
Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
 Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Sauti yake iliibua hisia hasa aliposena naipenda saana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote.
Bwana Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.

UINGEREZA IMEJITOA KATIKA - UK

Nchi ya Uingereza imejitoa kutoka katika jumuia ya UK. Matoakeo ni kama inavyoonekana hapo juu.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEZIREJESHA PESA KWA NEC

Rais Dkt. John Magufuli akipokea mfano wa hundi ya shilingi bilioni 2 kutoka kwa Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha kwa Rais Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa bakaa ya fedha hizo haikuathiri kwa namna yoyote uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
"Mheshimiwa Rais fedha ambazo tunakukabidhi, tulijibanabana sana, japo muda wenyewe ulikuwa mfupi lakini tulijibanabana sana bila kuathiri utendaji wa shughuli za uchaguzi, isije ikawa inatoa sura kwamba iliathiri, haikuathiri, na katika hali hiyo kama ambavyo wengi ni mashahidi, hatujisifii, lakini uchaguzi ulienda vizuri," amesema Jaji Mstaafu Lubuva.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amelikubali ombi hilo na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.
"Na mimi ningefurahi zaidi kama hilo jengo lingejengwa Dodoma, kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi hii, na hasa kwa sababu Dodoma ni katikati ya Tanzania" Amesisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia amelikubali pendekezo la tume hiyo la kuanzishwa kwa mfuko wa tume ya uchaguzi ambao utakuwa unakusanya fedha kila mwaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaofuata, badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusubiri mwaka wa uchaguzi ndipo zitengwe fedha zote za kugharamia uchaguzi huo.

Wednesday, June 22, 2016

Moise Katumbi ahukumiwa miaka 3 jela

Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya dola milioni 6.
Katumbi hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.
Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.

Tuesday, June 21, 2016

Bajeti ya JPM 2016/17

Bajeti ya Serikali 2016/ 2017 ni Trilioni 29.5.....Matumizi ya Kawaida ni Trilioni 17.7, Mikopo ni Trilioni 11.1. Bofya Hapa Kuona Vipaumbele Vilivyotajwa 

 Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano itaizidi ya Serikali ya Awamu ya Nne kwa Sh7.1 trilioni baada ya Waziri wa Fedha kutangaza sura ya bajeti ya mwaka 2016/17 inayoonyesha kutakuwa na makusanyo na matumizi ya Sh29.5 trilioni.
 

Sura hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatofautiana na iliyopita iliyokuwa ya Sh22.45 trilioni katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na kiwango cha fedha kitakachotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ambacho ni zaidi ya mara mbili ya fedha za eneo hilo katika bajeti iliyopita. 

Waziri wa Fedha, Dk Phillip Mpango alisema wakati akiwasilisha mapendekezo ya kiwango cha ukomo wa bajeti jijini Dar es Salaam jana kuwa kati ya fedha hizo, Sh18.46 trilioni, ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya bajeti yote, zitatokana na jumla ya mapato ya ndani yanayohusisha na halmashauri.


DR Congo warlord Bemba jailed over war crimes


Congolese ex-rebel leader Jean-Pierre Bemba has been jailed for 18 years following a landmark conviction at the International Criminal Court (ICC) for war crimes and sexual violence.
Bemba, a former vice-president of DR Congo, was convicted in March of crimes committed in the neighbouring Central African Republic (CAR) in 2002-2003.
He was accused of failing to stop his rebels from killing and raping people.
Bemba's lawyers have already said they will appeal against his conviction.

Judges announced sentences of between 16 and 18 years for five counts of rape, murder and pillaging, with the jail terms running concurrently. The eight years Bemba has already spent in custody will be deducted from his term

Who is Jean-Pierre Bemba?

  • A well-connected businessman and the son of prominent Congolese businessman Bemba Saolona
  • 1998: Helped by Uganda to form MLC rebel group in Democratic Republic of Congo
  • 2003: Becomes vice-president under peace deal
  • 2006: Loses run-off election to President Joseph Kabila but gets most votes in western DR Congo, including Kinshasa
  • 2007: Flees to Belgium after clashes in Kinshasa
  • 2008: Arrested in Brussels and handed over to ICC
  • 2010: Trial begins
  • 2016: Found guilty of war crimes and crimes against humanity