Bajeti ya JPM 2016/17
Bajeti ya Serikali 2016/ 2017 ni Trilioni 29.5.....Matumizi ya
Kawaida ni Trilioni 17.7, Mikopo ni Trilioni 11.1. Bofya Hapa Kuona
Vipaumbele Vilivyotajwa
Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano itaizidi ya Serikali ya
Awamu ya Nne kwa Sh7.1 trilioni baada ya Waziri wa Fedha kutangaza sura
ya bajeti ya mwaka 2016/17 inayoonyesha kutakuwa na makusanyo na
matumizi ya Sh29.5 trilioni.
Sura hiyo ya bajeti ya mwaka
2016/17 inatofautiana na iliyopita iliyokuwa ya Sh22.45 trilioni katika
maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na kiwango cha fedha kitakachotengwa kwa
ajili ya shughuli za maendeleo, ambacho ni zaidi ya mara mbili ya fedha
za eneo hilo katika bajeti iliyopita.
Waziri wa Fedha, Dk
Phillip Mpango alisema wakati akiwasilisha mapendekezo ya kiwango cha
ukomo wa bajeti jijini Dar es Salaam jana kuwa kati ya fedha hizo,
Sh18.46 trilioni, ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya bajeti yote,
zitatokana na jumla ya mapato ya ndani yanayohusisha na halmashauri.