CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea kitendo cha Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Peter Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani.
Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance Mwasajone.
Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo umeandikwa na mwalimu
mwenyewe, Jacob Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele ya wanafunzi
wake akiwa darasani shule ya msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu
wengine kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’ iliyotapakaa katika
eneo la shule hiyo akidai kuwa huo ni uchafu.