Wednesday, May 4, 2016

Atletico Madrid yatinga fainali ligi ya mabingwa

MADRID, SPAIN - APRIL 13:  Antoine Griezmann of Atletico Madrid celebrates scoring his penalty with team mates for his team's second goal during the UEFA Champions League quarter final, second leg match between Club Atletico de Madrid and FC Barcelona at the Vincente Calderon on April 13, 2016 in Madrid, Spain.  (Photo by Mike Hewitt/Getty Images)
Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munchen ya Ujerumani.
Atletico wakiwa na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza nchini Uhispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Xabi Alonso kwenye mechi ya Jumanne iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya mshambuliaji Antoine Griezmann kusawazisha na kuwa 1-1.
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres kuokolewa na mlinda mlango Manuel Neuer.
Matokeo ya jumla ya nusufainali hiyo yalimalizika sare 2-2 lakini Madrid wakasonga kwa kuwa na bao la ugenini.
Sasa Atletico watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu katika fainali mjini Milan tarehe 28 Mei.