Picha hapo juu inaonesha watu wakisubiri sukari katika duka moja hapa jijini Dar.
May 06
2016 Rais Magufuli alizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika
mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa
ukitoka Dodoma kwenda Arusha. Rais Magufuli alitoa maagizo kwa
wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja,
vinginevyo serikali itachukua hatua kali.
Sasa
taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU Valentine Mlolowa kuwa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya
suala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
TAKUKURU
ilitembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni
miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na
anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo, haya ndio waliyoyabaini…..
TAKUKURU
imebaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika
maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya
Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo
ili iweze kusambazwa