Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi
ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush, amesema kuwa
hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi wa Novemba.
Bwana Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.
Jeb
ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani
kuwa hatompigia kura Bwana Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi
ambayo imegawanya chama cha Republican.
Mnamo Alhamisi Spika wa
Bunge, Paul Ryan, alisema kuwa hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo
tajiri, ingawa atakutana naye juma lijalo. Hata hivyo Bwana Trump
ameungwa mkono na mgombezi wa Urais wa zamani Bob Dole aliyeshindwa
katika uchaguzi na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1996.