Thursday, May 5, 2016
Rais Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Migiro imefanyika leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Asha-Rose Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Akizungumza baada ya kuapishwa, Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.
Dkt. Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.