Mwanamuziki Justin Bieber ameshtakiwa kwa dola milioni 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu.
Nyota
huyo ametuhumiwa kuivunja simu ya Robert Earl Morgan baada ya kujaribu
kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa pombeKIsa hicxho kilitokea
katika kilabu ya Cle mjini Texas mwezi uliopita.Kulingana na mtandao wa TMZ,Justin Bieber alikasirishwa na kuchukua simu yake na kuivunja.
Thamani ya iPhone haifiki dola 100,000.
Lakini ameshtakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu simu hiyo ilikuwa na picha ambazo haziwezi kupatikana tena,ikiwemo picha za sherehe ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa bibi yake.
Morgan pia anadai kwamba alipoteza idad kubwa ya nambari zake za mawasiliano ya biashara.