Saturday, May 14, 2016

Burundi rebels Kagame on defense to help the nation rather than exacerbate them.


President of Rwanda Paul Kagame has denied the allegation made by the United Nations that his country continues to help the rebels in neighboring Burundi.

Mr Kagame has said that the problem of Burundi come from within the country and not exported.

Burundi has been gripped by the worst political crisis since President Pierre Nkurunziza determined to fight for another term last year.

It is a full year since President Nkurunziza kuepekua coup attempt.

Rwanda denied similar claims about supporting rebels in the preliminary report of the United Nations in February.

Mr Kagame has criticized the publishers of the report which is expected to be submitted in the Security Council of the United Nations later, saying his time would serve well to highlight the problems facing nations rather than exacerbate them.

Braza K wa Futuhi ni nani???



M-ulewe ndugu huyu na umahili wake katika uigizaji ndani ya FUTUHI....

Mwanamke wa Senegal ateuliwa katibu mkuu Fifa




Kwa mara ya kwanza katika historia, mwanamke ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), shirikisho ambalo kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na wanaume. Bi Fatma Samba Diouf Samoura kutoka Senegal, ndiye katibu mkuu mpya. Atasimamia shughuli za kila siku katika shirikisho hilo ambalo kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa limekabiliwa na tuhuma za ulaji rushwa. Ni mwanadiplomasia aliyehitimu ambaye kwa sasa amekuwa akihudumu kama mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa nchini Nigeria. Amefanya kazi UN kwa miaka 21. Bi Samoura amesema ni fahari kubwa sana kwake kuteuliwa kwenye wadhifa huo. Tangazo hilo limefanywa na rais wa FIFA Gianna Infantino katika kongamano kuu la FIFA linaloendelea Mexico. Aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke alipigwa marufuku kutojihusisha na shughuli zozote za soka kwa miaka 12 mapema mwaka huu.

Friday, May 13, 2016

@ Mabalozi wakereka sherehe ya Museveni





Bw Museveni ameongoza Uganda tangu 1986 Wanabalozi kutoka nchi za Magharibi waliondoka kwa hasira kutoka kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni siku ya Alhamisi. Wanabalozi hao kutoka Marekani, nchi za Ulaya na Canada waliondoka ghafla baada ya Bw Museveni kushutumu vikali Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mabalozi hao pia walikerwa na kuwepo kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir kwenye sherehe hiyo. Bw Bashir anasakwa na mahakama ya ICC kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya halaiki. Sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Museveni, ya tano tangu achukue madaraka mwaka 1986, ilihudhuriwa na viongozi kutoka Chad, Ethiopia, Kenya, Somalia, South Africa, South Sudan, Tanzania na Zimbabwe. Rais Yoweri Museveni aapishwa Akihutubu, Bw Museveni alisema ICC ni “kundi la watu bure” na akasema haiungi mkono tena. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Elizabeth Trudeau alisema: "Kutokana na kuwepo kwa Rais Bashir na matamshi ya Rais Museveni, ujumbe wa Marekani, pamoja na wawakilishi kutoka nchi za EU na Canada, waliondoka kutoka kwenye sherehe kuonyesha kutofurahishwa kwao (na vitendo hivyo).”

UN: Rwanda bado inasaidia waasi Burundi





Ripoti ya siri iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inaituhumu Rwanda kwa kuendelea kuwasaidia waasi wanaotaka kumtoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Rwanda imekuwa ikitoa mafunzo, ufadhili na usaidizi wa kimipango kwa waasi hao. Baadhi ya maafisa wan chi za Magharibi wamekuwa wakidhani hilo lilikoma baada ya kutolewa kwa ripoti nyingine mwaka jana, lakini ripoti hiyo inasema hali ni kinyume. Kamati ya Baraza la Usalama la UN inayoshughulika na vikwazo itajadili ripoti hiyo baadaye leo Ijumaa.

Wednesday, May 11, 2016

Rais Magufuli aenda Uganda:- Rais John Magufuli ameondoka leo jijini Arusha kwenda Kampala nchini Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni





Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 12 mwezi huu. Akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, Rais Magufuli amesindikizwa wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na viongozi wengine wa mikoa hiyo wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.

Tuesday, May 10, 2016

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akagua Daraja la Nyerere




Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.


Huduma ya mabasi ya mwendo wa kasi TZ





Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam. Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA. Kituo cha mabasi ya mwendo wa kasi Tanzania Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia maripota mjini humo kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari. Kituo cha mabasi ya BRT Tanzania Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT,alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria. Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi

MWALIMU WA NENO LA MUNGU, NDUGU CHRISTOPHER MWAKASEGE

MANA ni Huduma ya Neno la Mungu yenye makao yake makuu Arusha Tanzania. Huduma hii inaongozwa na Neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Yohana 21:17 "Yesu akamwambia,"Lisha kondoo zangu". Soma zaidi Bonyeza picha au read more..

Tumu-unge mkono Rais wetu mpenzi katika kazi anayo ifanyaaa



Monday, May 9, 2016

Sukari iliyofichwa Arusha yagawanywa

Tani 45 za sukari zilizobainika kufichwa katika ghala la mfanyabiashara Karimu Dakiki wa jijini Arusha zimegawiwa kwa watendaji wa kata 25 za jiji la Arusha
 
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu

Tani 45 za sukari zilizobainika kufichwa  katika ghala la mfanyabiashara Karimu Dakiki wa  jijini Arusha zimegawiwa kwa watendaji wa kata 25 za jiji la Arusha ili wazisambaze kwa wananchi katika kata hizo.

Zoezi hilo la kugawa sukari kwa watendaji wa kata hizo limesimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu.

Nkurlu amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la serikali la kukabilina na hujuma ya baadhi ya wafanyabiashara wanaosababisha uhaba wa sukari kwa maslahi yao binafsi.

Kwa upande wake Kaimu Afisa biashara wa jiji la Arusha, Godfrey Edward amesema bado kuna uhaba wa sukari hivyo bidhaa hiyo iliyogawawiwa  itapunguza makali ya uhaba.

Uongozi wa mkoa wa Arusha umeendelea kuwaonya wafanyabiashara wasio waaminifu kuacha kuficha sukari kwa lengo la kuwalangua wananchi kwa kuwauzia kwa bei ya juu.

Sechelela Kongola
08 May 2016