Friday, May 13, 2016

@ Mabalozi wakereka sherehe ya Museveni





Bw Museveni ameongoza Uganda tangu 1986 Wanabalozi kutoka nchi za Magharibi waliondoka kwa hasira kutoka kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni siku ya Alhamisi. Wanabalozi hao kutoka Marekani, nchi za Ulaya na Canada waliondoka ghafla baada ya Bw Museveni kushutumu vikali Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mabalozi hao pia walikerwa na kuwepo kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir kwenye sherehe hiyo. Bw Bashir anasakwa na mahakama ya ICC kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya halaiki. Sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Museveni, ya tano tangu achukue madaraka mwaka 1986, ilihudhuriwa na viongozi kutoka Chad, Ethiopia, Kenya, Somalia, South Africa, South Sudan, Tanzania na Zimbabwe. Rais Yoweri Museveni aapishwa Akihutubu, Bw Museveni alisema ICC ni “kundi la watu bure” na akasema haiungi mkono tena. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Elizabeth Trudeau alisema: "Kutokana na kuwepo kwa Rais Bashir na matamshi ya Rais Museveni, ujumbe wa Marekani, pamoja na wawakilishi kutoka nchi za EU na Canada, waliondoka kutoka kwenye sherehe kuonyesha kutofurahishwa kwao (na vitendo hivyo).”