Friday, May 13, 2016

UN: Rwanda bado inasaidia waasi Burundi





Ripoti ya siri iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inaituhumu Rwanda kwa kuendelea kuwasaidia waasi wanaotaka kumtoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Rwanda imekuwa ikitoa mafunzo, ufadhili na usaidizi wa kimipango kwa waasi hao. Baadhi ya maafisa wan chi za Magharibi wamekuwa wakidhani hilo lilikoma baada ya kutolewa kwa ripoti nyingine mwaka jana, lakini ripoti hiyo inasema hali ni kinyume. Kamati ya Baraza la Usalama la UN inayoshughulika na vikwazo itajadili ripoti hiyo baadaye leo Ijumaa.