Wednesday, May 11, 2016

Rais Magufuli aenda Uganda:- Rais John Magufuli ameondoka leo jijini Arusha kwenda Kampala nchini Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni





Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 12 mwezi huu. Akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, Rais Magufuli amesindikizwa wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na viongozi wengine wa mikoa hiyo wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.