Friday, June 24, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEZIREJESHA PESA KWA NEC

Rais Dkt. John Magufuli akipokea mfano wa hundi ya shilingi bilioni 2 kutoka kwa Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha kwa Rais Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa bakaa ya fedha hizo haikuathiri kwa namna yoyote uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
"Mheshimiwa Rais fedha ambazo tunakukabidhi, tulijibanabana sana, japo muda wenyewe ulikuwa mfupi lakini tulijibanabana sana bila kuathiri utendaji wa shughuli za uchaguzi, isije ikawa inatoa sura kwamba iliathiri, haikuathiri, na katika hali hiyo kama ambavyo wengi ni mashahidi, hatujisifii, lakini uchaguzi ulienda vizuri," amesema Jaji Mstaafu Lubuva.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amelikubali ombi hilo na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.
"Na mimi ningefurahi zaidi kama hilo jengo lingejengwa Dodoma, kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi hii, na hasa kwa sababu Dodoma ni katikati ya Tanzania" Amesisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia amelikubali pendekezo la tume hiyo la kuanzishwa kwa mfuko wa tume ya uchaguzi ambao utakuwa unakusanya fedha kila mwaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaofuata, badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusubiri mwaka wa uchaguzi ndipo zitengwe fedha zote za kugharamia uchaguzi huo.