Friday, May 6, 2016

Kesi ya Kitilya na wenzake Mahakama imetupilia mbali rufaa iliyowekwa na mkurugenzi wa mashitaka DPP

mahakama Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam leo imetupilia mbali rufaa iliyowekwa na mkurugenzi wa mashitaka DPP ya kupinga kufutwa shitaka la nane la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili Harry Kitilya na wenzake wawili Shose Sinare na Sioi Solomon.
Uamuzi huo umetolewa na jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam Moses Mzuna ambapo ametaja sababu za kutupilia mbali rufaa hiyo ni pamoja na rufaa yenyewe kuwa na dosari za kisheria huku akisema upande wa Jamhuri bado una nafasi ya kurekebisha hati ya mashitaka.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye DPP alitangaza kukata rufaa mahakama ya rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam ya kusema haina mamlaka ya kusikiliza rufaa yake.
April 27 mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ililfuta shItaka la nane la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili aliyewahi kuwa Kamishna Mkuu  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili Shose Sinare na  Sioi Solomoni ambapo ilisema hatua hiyo inatokana na kutokuwa wazi kwa kosa hilo kwani hakuna maelezo yanayoonyesha namna gani washtakiwa walivyotenda kosa.