Thursday, May 5, 2016

Mradi wa uendelezaji Jiji la Dsm unatarajia kuanza mwezi July

makonda
Mradi mkubwa wa uendelezaji wa Jiji la dsm-DMDP- katika Uboreshaji wa Miundombinu ya Barabara Mbadala,Mifereji ya kupitisha maji taka pamoja na Upanuzi wa mito ili kupunguza athari za mafuriko unatarajia kuanza mwezi july mwaka huu baada ya Benki ya Dunia kutoa kukubali kutoa cha dola za kimarekani Milioni 300.
Aidha Serikali pia imetoa kiasi cha Dola milion 25.5 katika Kuchangia mradi huo katika awamu ya kwanza ambapo utawezesha kujengwa kwa kiwango cha lami barabara mbadala kilometa 65.8,ujenzi na upanuzi wa mito kwa ajili ya kurahisisha Upitaji wa maji, kilometa 13.8 pamoja na upandishaji hadhi makazi ya wananchi mpango utakaochukua miaka mitano kukamilika awamu ya kwanza.
Mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda  Akizungumza na waandshi wa habari jijini dsm amesema mradi huo utaanza kutekelezwa baada ya makubaliano na maafisa kutoka benki ya dunia yalikyofanyika hivi karibu.
Aidha Bw,Makonda amezitaja kata 14 ambazo ni makazi yatakayopandishwa hadhi na kujengwa nyumba za kisasa pamoja na miundo mbinu ya barabara kuwa ni Tandale ,mburahati,mwanayamala,gongolamboto,kiwalani Ukonga,keko mtoni yombo vituka ,kijichi ambapo pia kata hizo zitajengewa barabara za lami na miondo mbuni ya kisasa ikiwemo taa za barabarani na kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatoa ushirikiano pindi mradi utakapoanza.