Monday, May 9, 2016
Rais Dkt Magufuli ashiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana Mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
ameshiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo
la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Padri Kiongozi Germin Longio...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Padri Kiongozi Germin Longio...
Sunday, May 8, 2016
Saturday, May 7, 2016
Mwalimu apigwa kofi na afisa elimu

CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea kitendo cha Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Peter Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani.
Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance Mwasajone.
Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo umeandikwa na mwalimu
mwenyewe, Jacob Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele ya wanafunzi
wake akiwa darasani shule ya msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu
wengine kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’ iliyotapakaa katika
eneo la shule hiyo akidai kuwa huo ni uchafu.
Bidhaa ya sukari yaadimika nchini Tanzania
Bidhaa ya sukari imeandimika nchini Tanzania, hii imeifanya serikali Sikivu ya Tanzania inayo ongozwa na Rais Dr. JPM kuagiza kufanyika kwa uchunguzi kwa wafanya biashara wanaficha bidhaa hiyo.
Picha hapo juu inaonesha watu wakisubiri sukari katika duka moja hapa jijini Dar.
Picha hapo juu inaonesha watu wakisubiri sukari katika duka moja hapa jijini Dar.
May 06
2016 Rais Magufuli alizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika
mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa
ukitoka Dodoma kwenda Arusha. Rais Magufuli alitoa maagizo kwa
wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja,
vinginevyo serikali itachukua hatua kali.
Sasa
taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU Valentine Mlolowa kuwa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya
suala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
TAKUKURU
ilitembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni
miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na
anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo, haya ndio waliyoyabaini…..
TAKUKURU
imebaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika
maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya
Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo
ili iweze kusambazwa
Nduguye Bush asema hatompigia kura Trump
Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi
ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush, amesema kuwa
hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi wa Novemba.
Bwana Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.
Jeb
ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani
kuwa hatompigia kura Bwana Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi
ambayo imegawanya chama cha Republican.
Mnamo Alhamisi Spika wa
Bunge, Paul Ryan, alisema kuwa hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo
tajiri, ingawa atakutana naye juma lijalo. Hata hivyo Bwana Trump
ameungwa mkono na mgombezi wa Urais wa zamani Bob Dole aliyeshindwa
katika uchaguzi na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1996.
Subscribe to:
Posts (Atom)