Saturday, April 30, 2016
Pembe za Ndovu zachomwa moto KENYA.
Rundo la pembe za ndovu zimechomwa moto mjini Nairobi, ikiwa ishara ya kutuma ujumbe mkali kwa dunia, kutaka mauaji ya tembo yasitishwe.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye ataongoza shughuli hiyo inayofanyika katika Mbuga ya Taifa ya Nairobi, ametaka biashara ya pembe za ndovu ipigwe marufuku, ili kuwanusuru tembo wasitoweke katika mazingira yao asilia.
Awali akizungumza katika mkutano uliowashirikisha marais wa Afrika na wanaharakati wa kuhifadhi mazingira, Kenyatta alisema kamwe hawatoruhusu tembo ambao amesema ni urithi muhimu waangamie.
Kwa ujumla zitachomwa tani 105 za pembe za ndovu, na tani 1.35 ya pembe za faru, hiyo ikiwa shehena kubwa zaidi katika historia kuwahi kuchomwa.
Pembe hizo zilitokana na wanyama 340 waliouawa ambapo Afrika inao ndovu wapatao 500,000, lakini wapatao 30,000 huuawa na majangili kila mwaka, kukidhi mahitaji ya soko la pembe za ndovu na faru barani Asia.